Thursday, 13 August 2015

          NAFASI YA VIJANA KUJIKWAMUA KIUCHUMI UKIW BADO MASOMONI
               Ni matumaini yangu kuwa ndugu msomaji wa Makala hii mzima na buheri wa afya, kama ilivyo ada tunaangazia masuala mbalimbali  yanayotuhusu sisi vijana ni katika namna ya kuhakikisha tunakua na mtazamo chanya katika jamii inayotuzunguka. Leo tutaangazia suala la kujikwamua kiuchumi hasa wakati vijana wanapokua  masomoni.
             Linaweza kuwa si jambo geni kwako kusikia wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini wanamiliki vitega uchumi, hiyo ni kuhakikisha tu wanafanya jitihada za kila namna kutoka kimaisha hususani ukizingatia suala la ajira nchini bado ni kitendawili kisicho na majibu.lakini pia katika kuhakikisha hawakosi fedha ya malazi wanapokua vyuoni.
             Tanzania kama ilivyo nchi nyingi za kiafrika zinazoendelea inakabiliwa na tatizo kubwa la ajira hasa ukizingatia tatizo la ajira kwa vijana linakadiriwa kuwa Zaidi ya vijana elfu 70,000 wanaohitimu kutoka vyuo vikuu ni asilimia kumi tu (10%) wanaopata nafasi ya ajira, kitu kinachosababisha vijana wengi wanaomaliza masomo yao ya elimu ya juu kubaki mitaani wakilalamika bila kazi.
          Kuna kilio ambacho kila unapogusia suala la ujasiliamari basi vijana wengi wa vyuo vikuu utasikia wakilia na kulalamikia suala la mitaji, Vijana wengi wana mawazo ya kufanya biashara, lakini wakifikia kwenye suala la mitaji wengi hukwama, wengi huamini kuwa wanahitaji mitaji ya million kadhaa ili kufanya biashara kitu ambacho kinarudisha harakati zao za kujikwamua kiuchumi nyuma
             Fikra hizo za vijana naweza sema si sahihi sana kwani unaweza kuanza hata na mtaji wa elfu ishirini mpaka laki moja na ukatoka pia, lakini pia unaweza tumia kipaji ulichonacho kutoka kimaisha, hapa ndipo ule usemi wa” tone na tone hujaza ndoo” unapochukua nafasi yake. Kitu cha msingi cha kuzingatia hasa wewe kama kijana ni kuwa na mipango madhubuti na endelevu katika shughuli zako
     Unaweza shangaa na kujiuliza mtu anawezaje kutoka kwa mtaji wa shilingi elfu ishirini? Hyo hiyo pesa ya matumizi unayopata kutoka nyumbani inaweza kukuinua kutoka ngazi moja hadi nyingine ya kimaendeleo Lakini haya yote yanawezekana ukiwa na mipango madhubuti, na yote haya tutapata kuyaangazia katika matoleo yanayofuata, usikose

Kwa maoni na ushauri: 0656 249607, au elvinecb@gmail.com. Asanteni.

0 comments:

Post a Comment