Maafisa wa kikosi maalum cha kupambana na magaidi wa Mali wamevamia hoteli iliyokuwa imetekwa na washambuliaji wa kigaidi hapo jana.
Raia wa kigeni wanne,kutoka Afrika Kusini Ukraine na Urusi wameokolewa.
Awali maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema kuwa katika makabiliano na washambuliaji hao watu wanane walifariki .
Waliofariki ni wanajeshi watano, mfanyikazi mmoja wa Umoja wa Mataifa na washambuliaji wawili.
Hoteli hiyo hutumiwa kwa wingi na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini humo wanaojulikana kama MINUSA.
Kwa masaa kadhaa, raia wa Ukraine, Urusi na Umoja wa Mataifa walikwama katika hoteli hiyo wakati mapigano yakiendelea .
Hata hivyo taarifa za baadaye zilielezea kuwa watu kadhaa, kukiwemo wageni watano waliokolewa na kikosi maalumu cha jeshi la Mali.
Raia mmoja wa Mali alisema kuwa shughuli za kudhibiti hali ya usalama ndani na nje ya hoteli hiyo zingali zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment