Wednesday, 19 August 2015

Ugonjwa wa kipindupindu ulioibuka siku chache katika jiji la Dar es Salaam waua watu watatu hadi sasa.
wagonjwa wawili walifariki kwa ugonjwa huo juzi na mmoja amefariki jana usiku hivyo kufanya idadi ya wagonjwa kufikia watatu wakati huo huo wagonjwa 34 hadi sasa wamelazwa katika  wodi maalum iliyoandaliwa na hospitali ya Mwananyamala jijini Dar Es Salaam ili kuhakikisha kama wana Ugonjwa huo.
Katika kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda alisema jana "Tunachokifanya ni kutoa elimu kwa wananchi kupitia mabwana na mabibi afya, ili kuhakikisha wagonjwa hawaongezeki, ikiwezekana kuzuia kabisa maambukizi mapya kwa namna yoyote ile.
Mganga mkuu wa wilaya ya Kinondoni Aziz Msuya Alisema kuwa kambi maalum kwa ajili ya wagonjwa hao ya mburahati ipo tayari na wameshahamishia ikiwa tayari na wagonjwa 11 kutoka Mwananyamala


Chanza: Mwananchi

0 comments:

Post a Comment