Kocha wa Manchester United Loius Van Gaal aonesha
furaha yake wazi wazi baada ya Memphis Depay kuiwezesha team hiyo kufunga
magori 3-1 dhidi ya Club brugge.
Katika mtanange huo uliopigwa katika dimba la old
Trafford Club brugge ndo ilikua ya kwanza kupata gori baada ya Mchezaji wa Man
U Michael Carrick kujifunga mnamo dak ya 8 ya mchezo.
Hata hivyo furaha ya gori hilo kwa timu ya Club
Brugge halikudumu kwa muda mrefu kwani mnamo dakika ya 13 mchezaji wa zamani wa
klabu ya PSV Memphis Depay alisawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1
Kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika M. Depay
aliongeza bao lingine kwa timu yake ya Man U, matokeo yaliyodumu hadi kipindi
cha kwanza kuisha.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya Man U
kushambulia na kutawala mchezo kwa muda mrefu hali iliyosababisha kupotea kwa
matumaini kwa timu ya Club Brugge kurudisha bao hilo. Wakati mchezo ukielekea
ukingoni kabisa Marouane Fellain alifunga gori la Tatu na kufanya mchezo
kumalizika kwa matokeo ya 3-1.
Hata ivyo kocha Louis Van Gaal amesema ana Imani na
ujasiri mkubwa kuwa wataendelea kupata ushindi na mchezaji huyo mpya katika
kikosi hicho ataendelea kuipatia mabao mengi Zaidi Man U. Ameongeza kuwa
ushindi huo ni hatua nzuri kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment