
Kwenye zile stori za
City to City,
Nation to Nation nimekutana na hii kutoka kwa
Chege Chigunda ambaye wiki 3 zilizopita nilikutana nae
South Africa na alikua ameenda kufanya kazi na mmoja wa wasanii wa kundi la Mafikizolo,leo nakusogezea nyingine kutoka kwa mkali huyo huyo anaewakilisha familia ya
Tmk Wanaume Family.
Chege aliposikika kwenye Amplifaya alisema kuwa mbali na kumshirikisha moja kati ya memba wa Mafikizolo pia ana kazi nyingine ambayo amempa Kolabo mkali anaechipukia kwa sasa Nigeria anaitwa Runtown,sasa hivi Chege yuko Nairobi na ameenda kwa ajili ya kazi moja tu ya muziki.

Muziki uliompeleka
Chege Nairobi si muziki wa kurekodi yeye hapana ni muziki ambao kaombwa na Nonini kufanya nae Kolabo,
Chege na
Nonini haitokua singo ya kwanza kusikika pamoja ipo singo pia waliyofanya pamoja inaitwa
Kila mmoja ambayo alishirikishwa pia na
Lady B.

Sasa hivi
Chege bado yuko
Nairobi kukamilisha kolabo ya
Nonini inayoitwa
Wanajishuku imerekodiwa studio zinazoitwa
Ingoma na upande wa video imeongozwa na Director anayeitwa
Willie kutoka +254 Kenya,nimepata baadhi ya picha mtu wangu.
0 comments:
Post a Comment